SERIKLI YATOA TSH BIL 787.4 MIKOPO ELIMU YA JUU

 

SERIKLI YATOA TSH BIL 787.4 MIKOPO ELIMU YA JUU

SERIKLI YATOA TSH BIL 787.4 MIKOPO ELIMU YA JUU

TANZANIA
Serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu 
imeendelea kuongeza fedha kwa ajili ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu hadi kufikia Shilingi bilioni 787.4 mwaka 2024/25 kutoka Shilingi bilioni 570 zilizotolewa mwaka 2021/22. 
Ongezeko hili la bajeti limewezesha kuongezeka kwa idadi ya wanufaika kutoka wanafunzi 177,925 mwaka 2021/22 hadi wanafunzi 248,331 mwaka 2024/25 sawa na ongezeko la asilimia 39.6
Vilevile, Serikali imeendelea kutekeleza kwa vitendo dhamira yake 
ya kutoa mikopo kwa ngazi ya elimu ya stashahada (Diploma) kwa kutoa mikopo yenye thamani ya Shilingi bilioni 19.95 kwa wanafunzi 7,534 wa fani za sayansi na ufundi kwa mwaka wa fedha 2024/25 ikiwa ni ongezeko la asilimia 177.6 ikilinganishwa na wanafunzi 2,714 waliopata mikopo hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/24. 
Aidha,  Serikali imeendelea kutoa ufadhili wenye thamani ya Shilingi bilioni 7.29 kwa wanafunzi 646 wa mwaka wa kwanza na wanafunzi wanaoendelea (shahada wa kwanza 674 na ngazi 
ya umahiri 80) wenye ufaulu uliojipambanua katika fani za Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati kupitia SAMIA Skolashipu