KITUO CHA KUFUA UMEME CHA HALE KUZALISHA MW 21 ZA UMEME

 

KITUO CHA KUFUA UMEME CHA HALE KUZALISHA  MW 21 ZA UMEME

KITUO CHA KUFUA UMEME CHA HALE KUZALISHA  MW 21 ZA UMEME

TANGA
Mradi wa kukarabati miundombinu ya kuzalisha umeme katika Kituo cha Hale Mkoani Tanga chenye uwezo wa kuzalisha MW 21  utekelezaji umefikia 74% ambapo uchimbaji wa handaki na ujenzi wa barabara mpya yenye urefu wa kilometa 1.3 umekamilika kwa asilimia 100.
Kwa upande wa kituo cha kupoza umeme, kazi zinazoendelea ni pamoja na ujenzi wa misingi ya transfoma, ujenzi wa ukuta wa kuzuia moto pamoja na ujenzi wa jengo la switch gear. 
Aidha, kazi zinazoendelea kwa upande wa power house ni uondoaji wa mitambo ya zamani pamoja na lifti ya kuingilia kwenye jengo la mitambo huku kiasi cha Shilingi Bilioni 54 kikitarajiwa kutumika hadi kukamilika kwake.