FAHAMU KINACHOENDELEA KWENYE MRADI WA SGR

 

FAHAMU  KINACHOENDELEA KWENYE MRADI WA SGR

FAHAMU  KINACHOENDELEA KWENYE MRADI WA SGR

TANZANIA
Serikali imeendelea  kutekeleza mradi wa ujenzi wa reli ya SGR kwa awamu ya kwanza na ya pili ambapo hadi kufikia Machi 2025, ujenzi wa reli ya SGR awamu ya kwanza ya kutoka Dar es Salaam – Mwanza yenye urefu kilomita 1,219 za njia kuu pamoja na ujenzi wa vipande viwili vya awamu ya pili vya Tabora -Kigoma (Km 506) na Uvinza - Musongati yenye urefu wa kilomita 240 za njia kuu (Tanzania Km156 na Burundi km 84) umeendelea kutekelezwa.
Aidha,hadi mwezi Machi 2025, utekelezaji wa kipande cha kwanza cha  kutoka Dar es Salaam – Morogoro (km 300) umefikia asilimia 99.72 na kazi zinazoendelea ni
ujenzi wa njia kuingia bandarini (port link)
umefikia asilimia 91.78 na ujenzi wa mifumo ya ishara, mawasiliano na umeme umefikia asilimia 99.98. 
Aidha, utekelezaji wa kipande cha pili cha
kutoka Morogoro – Makutupora (km 422) umefikia asilimia 97.98 na kazi zinazoendelea ziko katika hatua mbalimbali za utekelezaji ambazo ni pamoja na ujenzi wa vivuko vya juu umefikia asilimia 88.52, ujenzi wa stesheni umefikia asilimia 98.52,
na ujenzi wa uzio umefikia asilimia 95.12.
Utekelezaji wa kipande cha tatu cha kutoka Makutupora – Tabora (km 368) umefikia asilimia 14.53 na kazi zinazoendelea ni pamoja na usanifu wa kina ambao umefikia asilimia 54.98; ujenzi wa kambi; na ukataji wa miinuko na ujazaji mabonde pamoja na utwaaji wa ardhi. 
Halikadhalika, utekelezaji wa kipande cha
nne cha kutoka Tabora – Isaka (km 165) umefikia asilimia 6.65 ambapo kazi zinazoendelea ni pamoja na usanifu wa kina; utafiti wa udongo na miamba; ujenzi wa kambi, machimbo ya kokoto
pamoja na utwaaji wa ardhi.
Vilevile, utekelezaji wa kipande cha tano cha kutoka Mwanza – Isaka
(km 341) umefikia asilimia 63.16 na kazi
zinazoendelea ni usanifu wa kina; ujenzi wa tuta; majengo ya stesheni; madaraja na vivuko vya binadamu na wanyama; utandikaji wa reli; ujenzi wa mifumo ya mawasiliano na umeme pamoja na
utwaaji wa ardhi.