TSH BIL 69.243 ZAJENGA YADI & SAKAFU BANDARI YA KWALA
PWANI
Serikali imeendelea na ujenzi wa yadi na sakafu ngumu yenye ukubwa wa hekta tano katika Bandari Kavu ya Kwala kwa ajili ya kuhifadhi shehena za mizigo, pia imekamilisha ujenzi wa barabara ya zege yenye urefu wa kilomita 15.5 kutoka barabara kuu ya Morogoro hadi Bandari Kavu ya Kwala iliyopo katika mkoa wa Pwani ambapo utekelezaji wa mradio huo umetumia shilingi bilioni 69.243.