TSH BIL 76.58 ZAJENGA BARABARA YA MZUNGUKO DODOMA

TSH BIL 76.58 ZAJENGA BARABARA YA MZUNGUKO DODOMA

 TSH BIL 76.58 ZAJENGA BARABARA YA MZUNGUKO DODOMA

DODOMA
Jumla ya shilingi bilioni  76.58  zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje wa Jiji la Dodoma yenye urefu wa kilomita 112.3. (9.14 fedha za ndani na shilingi bilioni 67.44 fedha za nje).
Hadi sasa Ujenzi wa sehemu ya kwanza kutoka Nala - Veyula - Mtumba - Ihumwa Bandari Kavu yenye urefu wa kilomita 52.3  unaendelea, na sehemu ya pili kutoka Ihumwa Bandari Kavu - Matumbulu - Nala yenye urefu wa kilomita 60 upo katika hatua za ukamilishwaji.
Ujenzi wa barabara hizi mbili unatarajiwa kukamilika ifikapo Desemba, 2024  (sehemu ya kwanza) na Machi 2025 (sehemu ya pili)