MITAMBO 20 YA KUPIMA HALI YA HEWA YANUNULIWA

 

MITAMBO  20 YA KUPIMA  HALI YA HEWA YANUNULIWA

MITAMBO  20 YA KUPIMA  HALI YA HEWA YANUNULIWA

TANZANIA
Serikali imeendelea kununua na kufunga mitambo na vifaa vya hali ya hewa ikiwemo seti ya mitambo 20 ya kupima hali ya hewa inayojiendesha yenyewe (Automatic Weather Station – AWS) ambapo ufungaji wa mitambo hiyo unaendelea.
Aidha, seti ya mitambo15 ya kupima hali ya hewa kilimo (Agro – synoptic
station) imenunuliwa ambapo seti 10 za mitambo hiyo zimefungwa katika vituo vya Kibaha,Naliendele, Kilwa Masoko, Lyamungo, Mlingano,Hombolo, Matangatuwani, Kizimbani, Uyole na
Mbinga.
Mathalan, TMA iko katika hatua za mwisho za ununuzi wa mtambo wenye mfumo wa kisasa wa kuandaa utabiri ambao utengenezaji wake umekamilika nchini Ufaransa na kwa sasa
taratibu za kuusafirisha kuja nchini zinaendelea.