CHUO CHA USAFIRI WA ANGA KUJENGWA

 

CHUO  CHA USAFIRI WA ANGA   KUJENGWA

CHUO  CHA USAFIRI WA ANGA KUJENGWA

DAR ES SALAAM
Serikali kupitia Chuo cha Usafiri wa Anga cha Tanzania (Tanzania Civil Aviation Training Centre - CATC)  imepanga kutumia kiasi cha shilingi  bilioni 78.07  kwa ajili  ya ujenzi wa Chuo cha Kisasa cha Usafiri wa Anga (CATC)   katika  eneo la Banana Mkoani Dar es salaam ambapo ujenzi huo unatarajiwa kuanza mwezi Juni 2025 na utachukua miaka mitatu (3) na unalenga kuboresha miundombinu ya kutoa mafunzo kwa wataalam wa usafiri wa anga ndani na nje  ya nchi.
Mradi huo ni sehemu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), wa kukifanya CATC kuwa Kituo Mahiri (Centre of Excellence) kwa kutoa mafunzo ya hali ya juu katika nyanja za usalama wa anga, usafirishaji, Uongozaji wa anga, na usimamizi wa udhibiti.