MTAMBO WA TSH BIL 2.9 MAABARA YA MKEMIA MKUU
DODOMA
Serikali imefanya uwekezaji mkubwa na wa kisasa ikihusisha manunuzi ya mtambo mkubwa uliogharimu Sh bilioni 2.9 kwaajili ya kutumika katika Ofisi ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kuchakata sampuli mbalimbali.
Mtambo huo unachukua sampuli zaidi ya 200 kwa muda mmoja na matokeo kupatikana haraka muda usiozidi saa moja, lengo ni kurahisisha huduma kwa wawekezaji na wafanyabiashara, hii ni kwa mujibu wa mkurugenzi wa Huduma za Sayansi Jinai, David Elias.
Mtambo huo kwa sasa unapatikana makao makuu Dodoma lengo la kuweka huduma hiyo kati kati ya Nchi ni kuwawezesha watu wote kuweza kupata huduma hiyo.
