MABORESHO MAKUBWA KWENYE AFYA YAFANYIKA
TANZANIA
Serikali kwa mwaka wa fedha 2024/25 imefanya maboresho makubwa kwenye sekta ya afya kwa kujenga hospitali mbili (2) za Manispaa ya Temeke na Jiji la Dodoma, uendelezaji wa hospitali 22 ambao upo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.
Pia inatekeleza usimikaji wa mfumo wa kieletroniki kwa ajili ya usimamizi na uendeshaji wa vituo vya kutole huduma za Afya (Government of Tanzania Hospital Management Information System (GoT-HoMIS) katika vituo vya afya 21, ujenzi wa vichomea taka 10 ambapo vitatu (3) vimekamilika na saba (7) vipo hatua mbalimbali za utekelezaji.
Aidha, inatekeleza ujenzi wa vituo vya afya 162, ambapo vituo 29 vimekamilika na 133 ujenzi unaendelea, ujenzi wa nyumba 114 za watumishi wa afya ambapo nyumba nane (8) zimekamilika na
nyumba 106 zipo katika hatua mbalimbali, ujenzi na uendelezaji wa majengo 28 ya wagonjwa wa nje ambapo manne (4) yamemekamilika na yanatumika na 24 ujenzi
unaendelea.
Vilevile inatekeleza ujenzi na ukamilishaji wa zahanati 347 ambapo zahanati 28 zimekamilika na 319 utekelezaji upo katika hatua mbalimbali na ujenzi wa wodi 93 ambapo wodi 21 zimekamilika na 72 ujenzi unaendelea.