VIWANJA 12 VYA NDEGE VYAIMARISHWA MAWASILIANO
TANZANIA
Katika kuimarisha usalama wa usafiri wa anga, Serikali imeendelea kuboresha mawasiliano ya sauti baina ya mwongoza ndege na rubani ambapo ufungaji wa mitambo ya mawasiliano ya sauti umekamilika katika kituo mbadala cha mawasiliano kwa dharura (Back-up Center) pamoja na viwanja vya ndege 12.
Viwanja hivyo ni Julius Nyerere International Airport (JNIA), Pemba, Abeid Amani Karume International Airport (AAKIA), Kilimanjaro (KIA), Tanga, Dodoma, Arusha, Tabora, Kigoma, Mtwara, Mwanza na Songwe.