VITONGOJI 82 TARIME VIJIJINI KUPELEKEWA UMEME

 

VITONGOJI 82 TARIME VIJIJINI KUPELEKEWA UMEME

VITONGOJI 82 TARIME VIJIJINI KUPELEKEWA UMEME 

MARA
Vitongoji 82 ambavyo bado havijafikiwa na umeme katika Wilaya ya Tarime mkoni Mara vitapelekewa umeme kupitia Mradi wa Kupeleka Umeme Vitongojini Awamu ya Pili B (HEP IIB) ambapo tayari zabuni ya kuwapata wakandarasi wa mradi huo imeshatangazwa na inatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni.
Jimbo la Tarime Vijijini lina jumla ya Vitongoji 500 ambapo vitongoji 225 tayari vina umeme, vitongoji 52 Wakandarasi wanaendelea na kazi, na vitongoji 82 zabuni ya kuwapata Wakandarasi imetangazwa kupitia Mradi wa Kupeleka Umeme Vitongojini Awamu ya Pili B(HEP IIB) na vitongoji 141 vilivyosalia vitaendelea kupelekewa umeme kupitia miradi ijayo.
Aidha, serikali kupitia  mpango wa kuunganisha Umeme katika taasisi mbalimbali kupitia fedha za mradi wa Covid 19, imeshaanza kutekeleza mpango huo ambapo mpaka sasa zaidi ya taasisi 3000 zimeshaunganishwa na umeme zikiwemo taasisi za Elimu, Afya, Dini, Migodi pamoja na visima vya maji.