TSH TRIL 1.59 ZAFIKISHA UMEME VIJIJI 4071

 

TSH TRIL 1.59  ZAFIKISHA UMEME VIJIJI 4071

TSH TRIL 1.59  ZAFIKISHA UMEME VIJIJI 4071

TANZANIA
Serikali imeunganisha umeme katika vijiji 4,071 kwa gharama ya sh. trilioni 1.593 na hivyo kuwezesha vijiji vyote 12,318 vya Tanzania Bara kuunganishwa na umeme.
Aidha hatua inayofuata baada ya kukamilisha mradi wa kupeleka umeme katika vijiji vyote ni  kupeleka umeme kwenye vitongoji ambapo jumla ya vitongoji 33,657 kati ya 64,359, sawa na asilimia 52.3 vimeunganishwa na huduma ya umeme.
MUHIMU:- Usambazaji wa umeme katika vijiji na vitongoji utawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi hususan zinazohitaji nishati ya umeme zikiwemo kuchomelea vyuma, useremala, kuchakata nafaka na kuchenjua madini.