MASOKO & VITUO VYA UNUNUZI MADINI VYAONGEZEKA
SHINYANGA
Jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali kupitia sekta ya madini imefanikisha kuongezeka kwa masoko na vituo vya ununuzi wa madini kutoka 41 na 61 mwaka 2020/2021 hadi kufikia 42 na 100 mwaka 2023/2024 ambapo kulifanyika biashara ya madini yenye thamani ya shilingi 2,095,960,697,019.40 na shilingi 1,926,415,580,991.11 mtawalia.
Aidha, Serikali imenunua mitambo mitano (5) ya uchorongaji kwa ajili ya wachimbaji wadogo na kuigawanya kwenye maeneo mbalimbali ya uchimbaji mdogo wa madini nchini
Pia ili kuendeleza Madini Muhimu na Madini Mkakati, Serikali imetoa leseni ya uchimbaji mkubwa wa madini Tembo (Heavy Mineral Sands) kwa mradi wa Tajiri uliopo Wilaya ya Pangani, Mkoa wa Tanga pamoja na Leseni ya Ujenzi wa Kiwanda cha Kusafisha Madini ya Metali Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga
