RAIS WA MSUMBIJI MHE.CHAPO KUANZA ZIARA NCHINI
TANZANIA
Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Mhe. Daniel Francisco Chapo anatarajia kuanza Ziara ya Kiserikali nchini kwa siku 3 kuanzia Mei 7 hadi 9,2025 kufuatia mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan.
Hii ni ziara ya kwanza kwa Mhe.Chapo kuifanya nchini tangu alipoapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Januari 15,2025
Mhe. Rais Dkt Samia atampokea Rais Chapo Mei 8 Ikulu Jijini Dar es salaam ambapo watafanya mazungumzo rasmi pamoja na kushuhudia uwekaji Saini wa mikataba na hati za makubaliano (MOu) Katika sekta mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha ushirikiano
Aidha Mhe.Rais Chapo akiwa nchini atapata fursa ya Kutembelea hospital ya Taifa Muhimbili, kituo Cha urithi Cha ukombozi Cha Afrika,mradi wa kimkakati wa reli ya kisasa (SGR) pamoja na Kutembelea Zanzibar ambako atafanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na mwenyekiti Baraza la mapinduzi Mhe.Hussein Ali Mwinyi na Kutembelea miradi mbalimbali ikiwemo mamlaka ya kusimamia uvuvi wa bahari kuu na Soko la samaki Malindi.