UKARABATI BARABARA MTWARA- MINGOYO=MASASI KUANZA
MTWARA
Serikali ipo katika hatua za mwisho kuanza ukarabati kwa kiwango cha lami wa barabara ya Mtwara – Mingoyo – Masasi (km 200.51) ambapo mikataba ya ujenzi wa sehemu za Mtwara – Mingoyo (km 82.27) na Mingoyo – Nanganga – Masasi (km 118.24) imesainiwa.