BARABARA, MADARAJA VYAJENGWA BAJETI 2024/25
TANZANIA
Hadi Aprili, 2025 jumla ya kilometa 98.13 za barabara za mikoa zimejengwa kwa kiwango cha lami na kilometa 192.9 zimekarabatiwa kwa kiwango cha changarawe ( kutoka kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2024/25).
Aidha, ujenzi/ukarabati wa madaraja madogo 7 kwa kutumia fedha za Mfuko Mkuu wa Serikali na 9 kwa kutumia fedha za Mfuko wa Barabara umekamilika na madaraja 91 yapo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.