TSH MIL 322.07 ZAONGEZA MAJI ITAGUTWA
IRINGA
Kiasi cha Shilingi milioni 322.07 kimetumika kutekeleza mradi wa maji wa Itagutwa, uliotekelezwa na Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) mkoa wa Iringa.
Mradi wa Itagutwa ni upanuzi wa skimu ya awali iliyokuwa ikihudumia Kijiji cha Kinywang’ang’a kwa kutumia chanzo cha maji kutoka Kijiji cha Itagutwa.
Kupitia upanuzi huu, uwezo wa uzalishaji maji umeongezeka hadi kufikia lita 10,440 kwa saa, sawa na lita 250,560 kwa siku. Hii ni zaidi ya mara mbili ya mahitaji ya sasa ya maji kwa siku katika eneo hilo, ambayo ni lita 108,030, hivyo kuweka msingi imara wa huduma endelevu kwa jamii hiyo.
Aidha Kwa sasa, mradi unahudumia moja kwa moja wakazi 1,645 wa Kijiji cha Itagutwa, ambao hapo awali walikumbwa na changamoto ya kutumia muda mwingi kutafuta maji, hali iliyokuwa ikipunguza ufanisi katika shughuli zao za kijamii na kiuchumi.
Utekelezaji wa mradi ulianza rasmi mwezi Mei 2023 na ulikamilika ndani ya miezi sita kama ilivyopangwa.
