MEGAWATI 165 ZA UMEME MBAGALA ZAFIKIA 70%
DAR ES SALAAM
Kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Mbagala Mkoani Dar es salaam chenye megawati 165 kutoka Megawati 45 za awali kwa sasa utekelezaji wake umefikia asilimia 70 ambapo kiasi cha shilingi bilioni 1.728 kinatumika kukamilisha mradi huo.
Ongezeko hilo ni mara mbili ya uwezo wa awali (kutoka megawati 45 hadi 165) ambapo kukamilika kwake kutasaidia kuondoa kabisa changamoto ya kukatika kwa umeme katika maeneo hayo na viunga vyake.
