TSH BIL 4+ KWENYE MAJI MIRERANI

 

TSH BIL 4+ KWENYE MAJI MIRERANI

TSH BIL 4+ KWENYE MAJI MIRERANI

MANYARA
Serikali inatumia kiasi cha shilingi 4,373,838,884.62 kutekeleza  mradi wa kuboresha huduma ya majisafi katika Mji wa Mirerani mkoani Manyara. 
Mradi unahusisha ulazaji wa bomba kutoka kwenye kisima kipya MV1 mpaka kwenye tanki jipya umbali wa kilomita 11.592; ulazaji wa mabomba ya kusambaza maji umbali wa kilomita 45; ujenzi wa tanki la lita milioni moja; ujenzi wa jengo la mitambo; upelekaji wa umeme  kwenye chanzo; ujenzi wa jengo la kutolea huduma; ukarabati wa tanki la lita 150,000; na ujenzi wa chemba 12.
Hadi mwezi Aprili 2025, utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 75 na kazi 
zilizotekelezwa ni ulazaji wa bomba kutoka kwenye kisima kipya MV1 mpaka kwenye tanki jipya umbali wa kilomita 
10.862; na ulazaji wa mabomba ya kusambaza maji umbali wa kilomita 45. 
Mradi unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba, 2025 na kunufaisha wananchi wapatao 57,600.