FAHAMU KUHUSU MIRADI YA BARABARA 202425

 

FAHAMU KUHUSU MIRADI YA BARABARA 2024/25

FAHAMU KUHUSU MIRADI YA BARABARA 2024/25

TANZANIA
Serikali katika mwaka wa fedha 2024/25, ilipanga kutekeleza  miradi 385ya barabara kuu kwa kiwango cha lami na kukarabati kilometa 35 kwa kiwango cha lami, ujenzi wa madaraja 17, ukarabati wa daraja moja (1).
Hadi kufikia Aprili, 2025, ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara zenye urefu wa kilometa 109.49 umekamilika na ujenzi wa kilometa 275.51 unaendelea huku maandalizi ya ujenzi wa madaraja tisa (9) na Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina wa madaraja mawili (2) ukiendelea.
Aidha, ujenzi wa madaraja matano (5) unaendelea na ujenzi wa madaraja matano (5) upo katika hatua za maandalizi.
Vilevile, taratibu za ununuzi ya Makandarasi wa ujenzi wa madaraja matano (5) zinaendelea. 
Kadhalika, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa madaraja 11 katika mikoa mbalimbali nchini.