TSH BIL 1.9 ZABORESHA KAMPASI ZA LITA
DODOMA
Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassan imetumia kiasi cha shilingi bilioni 1.9 kwa ajili ya ujenzi wa majengo na ukarabati wa kampasi za Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo nchini (LITA),Mpwapwa mkoani Dodoma.
Katika hatua nyingine serikali pia imetoa kiasi cha shilingi milioni 168 kwa ajili ya ukarabati wa mabweni mawili ya kampasi ya Temeke mkoani Dar es Salaam.
Mbali na ujenzi wa majengo ya wakala huo imeanza ujenzi wa kampasi nyingine mkoani Songwe utakaogharimu shilingi bilioni 1.2 hadi kukamilika kwake