FAHAMU KUHUSU MIRADI YA MWENDOKASI INAYOTEKELEZWA
DAR ES SALAAM
Serikali inaendelea na utekelezaji wa miradi ya magari yaendayo kasi (Mwendokasi) katika maeneo mbalimbali jiji la Dar essalaam.
Miradi inayoendelea kutekelezwa ni pamoja na:
i.Ujenzi wa Barabara za Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya III kutoka Maktaba – JNIA - Gongolamboto (km 23.3)
ii.Ujenzi wa Barabara za Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya IV kutoka Maktaba – Morocco – Mwenge - Tegeta na Mwenge - Ubungo (km 30.1); na
iii. Maandalizi ya kuanza ujenzi wa Barabara za Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya V kutoka Ubungo – Bandarini, Makutano ya Tabata – Tabata Segerea na Tabata – Kigogo (km 27.6).
Aidha, Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina kwa ajili ya ujenzi wa barabara za juu katika makutano ya Buguruni (Mandela/Uhuru), Magomeni, Fire, Ally Hassan Mwinyi/UN, Ally Hassan Mwinyi/ Kinondoni, Mwenge na Morocco umekamilika.
Kadhalika,Serikali kupitia wizara ya Ujenzi inaendelea na majadiliano na JICA ili kuweza kufadhili ujenzi wa flyovers mbili katika makutano ya barabara ya Ally Hassan Mwinyi na Sam Nujoma (Mwenge) pamoja na makutano na barabara ya Kawawa (Morocco).