HOSPITALI ZOTE KONGWE KUKARABATIWA

 

HOSPITALI ZOTE KONGWE KUKARABATIWA

HOSPITALI ZOTE KONGWE KUKARABATIWA

DODOMA
Serikali kupitia Ofisi ya Rais – TAMISEMI  itaendelea kukarabati hospitali zote Kongwe kupitia mpango mkakati wa ukarabati, na upanuzi wa hospitali kongwe za halmashauri ,vituo vya afya Pamoja na zahanati ili kuboresha miundombinu ya huduma za afya kote nchini.
Tayari serikali imeweka mpango mkakati wa ukarabati na upanuzi wa vituo vyote kongwe vya kutolea huduma za afya, ambapo tayari ukarabati na upanuzi umeanza katika ngazi ya hospitali kongwe za halmashauri, na baada ya hospitali za halmashauri, vitafuata vituo vya afya na zahanati zote kongwe ambazo zinahitaji ukarabati.