MITAMBO YA HALI YA HEWA YAFUNGWA IRINGA NA BUKOBA TANZANIA
Serikali imekamilisha ufungaji wa mitambo miwili (2) ya kutoa huduma za hali ya hewa katika viwanja vya ndege vya Iringa na Bukoba, hatua hii imekuja ili kuboresha huduma za hali ya hewa kwenye sekta ndogo ya usafiri wa anga.
Aidha, TMA imefanyiwa ukaguzi wa kimataifa wa utekelezaji wa mfumo wa kudhibiti ubora wa huduma za hali ya hewa zinazotolewa katika sekta ya usafiri wa anga kuanzia tarehe 03 hadi 14 Machi, 2025.
Kutokana na ufanisi uliobainika, TMA imeendelea kukidhi vigezo vya kumiliki cheti cha ubora (ISO 9001: 2015) katika sekta ya usafiri wa anga.