KINACHOENDELEA BANDARI YA KISIWA MGAO

 

KINACHOENDELEA BANDARI YA KISIWA MGAO

KINACHOENDELEA BANDARI YA KISIWA MGAO 

MTWARA
Serikali kupitia  Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (Tanzania Ports Authority -TPA) imeendelea na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Gati jipya na Conveyer belt katika Bandari ya Kisiwa Mgao mkoani Mtwara ambapo  Kiasi cha shilingi bilioni 434.5 kinatumika kwa ajili ya ujenzi wa  Bandari hiyo ambapo itakapokamilika itahudumia shehena chafu (dirty cargo) kama vile makaa ya mawe na saruji. 
Utekelezaji wa mradi huo umeanza  tarehe 3 Januari 2025 na unatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 3 Julai 2027 na unatekelezwa na kampuni ya China, M/S China Harbour Engineering Company Limited (CHEC).
Bandari ya Kisiwa-Mgao inatarajiwa kuwa kiungo muhimu katika kuimarisha sekta ya uchukuzi na kuleta maendeleo ya kiuchumi katika eneo hilo na taifa kwa ujumla.
Lengo la mradi huu ni kuiwezesha bandari ya Mtwara iendelee kutoa huduma kwa ufanisi bila kuathiri mazingira.