JNIA NA AAKIA VYABORESHEWA MIFUMO HALI YA HEWA
DAR ES SALAAM
Serikali kupitia Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) hadi kufikia Machi,2025 TCAA imefanikisha Kufunga mifumo ya kutoa taarifa za hali ya hewa kwa njia ya sauti ya redio (DATIS) katika viwanja vya ndege vya Julius Nyerere (JNIA) na Abeid Amani Karume (AAKIA).
Utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 60, ambapo JNIA kazi ya ufungaji, mafunzo kwa wataalam na upokeaji wa mradi (Site acceptance) yamekamilika na shehena ya mitambo kwa ajili ya Kiwanja cha AAKIA inatarajiwa kuwasili kabla ya mwishoni mwa mwezi Mei 2025.