KAZI INAENDELEA KWENYE BANDARI YA KWALA

 

KAZI INAENDELEA KWENYE BANDARI YA KWALA

KAZI INAENDELEA KWENYE BANDARI YA KWALA

PWANI
Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea na utekelezaji wa ujenzi wa Bandari Kavu ya Kwala  iliyopo Vigwaza, Kibaha, mkoani Pwani, ambapo utekelezaji wa ujenzi wa barabara ya zege yenye urefu wa kilomita  15.5 kutoka barabara kuu ya Morogoro hadi Bandari Kavu ya Kwala umekamilika.
Ujenzi wa uzio wenye mzunguko wa kilomita 2.9 umekamilika, mtandao wa reli ya MGR wenye urefu wa kilomita 1.3 umekamilika na ujenzi wa yadi ya sakafu ngumu (pavement) yenye ukubwa
wa hekta tano (5) kwa ajili ya kuhifadhi shehena unaendelea na utekelezaji wake umefikia asilimia 96.6.
Bandari Kavu hii imeanza kutoa huduma kwa kupokea makasha kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwa kutumia njia ya reli na barabara.
Katika kutekeleza mkakati wa kuboresha biashara baina ya Tanzania na nchi za kikanda na kulifanya eneo la Kwala kuwa la kimkakati zaidi, Serikali ilitoa
maeneo kwa ajili ya kuhudumia shehena ya nchi za Rwanda, DRC, Burundi na Zambia. 
Aidha, Serikali imetenga maeneo kwa ajili ya nchi za Uganda, Malawi, Sudan Kusini na Zimbabwe. Nchi hizo kwa sasa zimeanza uendelezaji wa maeneo hayo ambapo Burundi imeanza ujenzi wa uzio na DRC inakamilisha Upembuzi Yakinifu.