MHE.RAIS SAMIA ATUMA SALAMU ZA POLE KIFO CHA CHARLES HILARY

 

MHE.RAIS SAMIA ATUMA SALAMU ZA POLE KIFO CHA CHARLES HILARY

MHE.RAIS SAMIA ATUMA SALAMU ZA POLE KIFO CHA CHARLES HILARY

DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametuma Salamu za pole kufuatia taarifa za kifo za Bwana Charles Hilary aliyekuwa Mkurugenzi wa idara ya mawasiliano Ikulu  Zanzibar na msemaji mkuu wa serikali ya mapinduzi Zanzibar.
Kupitia mitandao ya Kijamii Mhe.Rais Samia ameandika"Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Bw. Charles Hilary, Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu Zanzibar kilichotokea leo Mei 11, 2025.
Ninatoa pole kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Mwinyi, familia, ndugu, jamaa na marafiki na wadau wote wa sekta ya habari nchini kwa msiba huu.
Ndugu Charles Hilary atakumbukwa kwa mchango wake adhimu wa zaidi ya miaka 40 katika kukuza sekta ya habari nchini tangu akiwa redioni hadi kwenye televisheni, pamoja na unasihi kwa wanahabari wachanga.
Namuomba Mwenyezi Mungu aijaalie familia yake uvumilivu na subra katika kipindi hiki kigumu, na ailaze roho ya mpendwa wetu mahala pema.
Hakika sote ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake tutarejea"
Bimkubwa Tanzania tunaungana na Mhe.Rais Dkt Samia kuwapa pole wote walioguswa na msiba huu, Mungu amlaze marehemu mahali pema peponi.