FAHAMU KUHUSU BANDARI YA MWANZA KASKAZINI
MWANZA
Serikali inaendelea na uboreshaji wa Bandari ya Mwanza Kaskazini ambapo kiasi cha shilingi bilioni 18.6 kinatumika huku maboresho hayo yakihusisha upanuzi wa gati kutoka mita 98 hadi 115 pamoja na jengo la ghorofa la abiria namradi huu umefikia asilimia 58.
Aidha serikali inatarajia kuanza uboreshaji wa Bandari ya Mwanza kusini mara baada ya kukamilika kwa baadhi ya miundombinu ya Bandari ya Mwanza kaskazini ili kutoathiri shughuli za kibandari.
Maboresho haya yatawezesha kuhudumia melikubwa kama vile MV. Mwanza inayotarajiwa kutoa huduma katika Ziwa Victoria.