BARABARA TAMCO-VIKAWE-MAPINGA WAFIKIA 60%
PWANI
Ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya TAMCO – Vikawe – Mapinga (km 24) Mkoani Pwani unafanyika kwa awamu ambapo ujenzi wa kilometa 4.7 umekamilika na ujenzi wa kilometa 3.6 umefikia asilimia 60.
Aidha, ujenzi wa sehemu ya Pangani – Mapinga (km 13.59) umefikia asilimia 11.
Vilevile, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami barabara ya Makofia – Mlandizi (km 36.7).