RAIS WA NAMIBIA MHE. DKT NETUMBO NANDI-NDAITWAH KUFANYA ZIARA NCHINI
DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Namibia Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah anatarajia kufanya ziara ya kiserikali ya siku mbili nchini Tanzania kuanzia (leo) Mei 20 hadi 21, 2025 kufuatia mwaliko aliopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Hii ni ziara ya kwanza ya Mhe. Nandi-Ndaitwah kuifanya hapa nchini tangu alipoapishwa kuwa Rais wa Namibia tarehe 21 Machi 2025 na inalenga kukuza ushirikiano wa kisiasa, kiuchumi na kijamii ikiwemo katika nyanja za kibiashara, uwekezaji na elimu.
Tutakuletea matangazo ya moja kwa moja , tufuatilie kwenye mitandao yetu yakijamii facebook, x, instagram, Tiktok na Youtube @Bimkubwatanzania.