"UCHAGUZI UTAFANYIKA KWA UTULIVU NA AMANI" DKT SAMIA
DODOMA
Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesema serikali imejipanga katika kuhakikisha uchaguzi utafanyika katika mazingira ya utulivu na amani ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu.
Rais Samia ametoa kauli hiyo April 25, 2025 wakati akilihutubia Taifa kupitia vyombo vya habari Ikulu ya Chamwino Ikiwa ni siku moja kuelekea miaka 61 ya Muungano tarehe 26, April.
"Tutafanya kila tuwezalo kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika kwenye mazingira ya utulivu na amani katika kipindi chote cha matayarisho hadi wakati wa uchaguzi ili kuwa na uchaguzi huru na wa haki"Amesema Mhe.Rais Samia
Aidha Mhe.Rais Dkt Samia ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kushiriki katika mchakato mzima wa uchaguzi kuanzia kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura, kugombea hadi kupiga kura .
Vilevile Mhe. Rais Samia amewataka viongozi, wanachama na wafuasi wa vyama vya siasa kuzingatia taratibu na sheria za nchi ili uchaguzi huu uwe fursa ya kuimarisha umoja na demokrasia ili tupate viongozi walio bora na imara.
#MIAKA61YAMUUNGANO