UBORESHAJI TAASISI YA TIBA YA MIFUPA NA UBONGO MUHIMBILI (MOI)

 

UBORESHAJI TAASISI YA TIBA YA MIFUPA NA UBONGO MUHIMBILI (MOI)

UBORESHAJI TAASISI YA TIBA YA MIFUPA NA UBONGO MUHIMBILI (MOI)

Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imepiga hatua kubwa katika kuboresha huduma zake, hususan kwa kupanua wigo wa huduma za kibobezi zikiwemo uchunguzi na upasuaji wa ubongo, nyonga na magoti, pamoja na upasuaji wa migongo kwa njia ya kufungua.
Katika kipindi cha miaka minne uwekezaji mkubwa umefanyika katika mafunzo na utafiti, hali ambayo imechangia ongezeko la wataalam waliobobea katika sekta ya mifupa na mishipa ya fahamu na hatua hiyo imeongeza ufanisi wa matibabu yanayotolewa kwa wagonjwa.
MOI imehudumia jumla ya wagonjwa 816,400, huku zaidi ya wagonjwa 7,000 wakinufaika moja kwa moja na huduma za kibobezi.
Aidha, katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Dkt Samia MOI imepokea mradi wa kufua hewa ya oksijeni wenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.7 ambao unatarajiwa kuokoa Shilingi Milioni 1.2 zilizokuwa zikitumika kununua oksijeni hiyo kila mwaka.
MOI pia imefanikiwa kutekeleza mpango wa “Tiba Mkoba” mpango unaolenga kuwafikia wananchi walioko maeneo ya mbali na kuwapatia huduma za kibobezi. Kupitia mpango huo, jumla ya wagonjwa 4,496 wamepatiwa huduma za kibingwa bila kulazimika kusafiri umbali mrefu kutafuta matibabu.
#BimkubwanaAfyaKazini