TSH BIL 88.725 ZINAJENGA KM 50 KIBAONI-MLELE
KATAVI
Kiasi cha shilingi bilioni 88.725 kinatekeleza ujenzi wa barabara ya Kibaoni – Sitalike, sehemu ya kwanza ya Kibaoni – Mlele (km 50) kwa kiwango cha lami katika Halmashauri ya Mpimbwe mkoani Katavi.
Miradi mingine inayoendelea kutekelezwa katika Hlamshauri hiyo ni Barabara Vikonge – Luhafwe (km 25) ambao upo 57.4% na unagharimu Sh bilioni 35.6, barabara ya Luhafwe – Mishamo (km 37) upo 10% ya utekelezaji na unagharimu Sh bilioni 58.3 pamoja na barabara inayoelekea Bandari ya Karema kutoka Kagwira zaidi ya kilometa 112 Mkandarasi ameshapatikana na mwaka huu barabara hiyo itaanza kujengwa kwa kiwango cha lami.
#TukutaneKatavi