HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

 

HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

Serikali katika kipindi cha miaka minne imefanya maboresho makubwa kwenye sekta ya afya, ikiwemo miundombinu, dawa na vifaa tiba.

Hospitali ya Taifa Muhimbili yenye kampasi mbili na Hospitali ya Rufaa ya Kitaifa na kubwa kuliko zote nchini ina vitanda 2,043 ambapo Upanga kuna vitanda 1,435 na Mloganzila vipo 608. Katika kampasi zote mbili wagonjwa 4,000 wanaonwa kwa siku.

Serikali imedhamiria kutumia kiasi cha shilingi trilioni 1.2  kuboresha Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kuijenga upya ili kuwezesha huduma zote kutolewa ndani ya jengo moja litakalokuwa na vitanda 1,757 kutoka 1,435 vya sasa, na mradi huo ni ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania na Korea Kusini.

Utekelezaji wa mradi huo ni wa awamu moja ambao utachukua miaka mitano kukamilika baada ya kusaini mkataba na mradi huu wa kihistoria katika sekta ya afya nchini na Ukanda wa Afrika, utakuwa na faida lukuki ikiwemo kuboreshwa kwa huduma za kibingwa na ubingwa bobezi kupitia vifaa tiba vya kisasa na kwamba Serikali itapunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya fedha kusafirisha wagonjwa nje ya nchi, kuwezesha wagonjwa kupata huduma zote katika eneo moja, kupunguza mizunguko na usumbufu pamoja na kuwa na mpangilio mpya wa hospitali huku eneo kubwa likibaki wazi kwa matumizi ya maendeleo mengine miaka 50 ijayo