MHE.RAIS SAMIA ASAMEHE WAFUNGWA 4887
MHE.RAIS SAMIA ASAMEHE WAFUNGWA 4887
DODOMA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa msamaha kwa wafungwa 4887 ambapo 42 kati yao wanaachiliwa huru leo tarehe 26 April na wengine 4845 wanabaki gerezani kumalizia sehemu ya kifungo kilichobaki baada ya kupewa msamaha huu.
Msamaha huu umewahusu wafungwa wa makundi mbalimbali ikiwemo:-
a. wafungwa wagonjwa wenye magonjwa ya kudumu au sugu ambao wapo kwenye hatua ya mwisho
b. wafungwa wote waliohukumiwa na mahakama kutumikia vifungo vya maisha gerezani wabadilishiwe vifungo vyao na kuwa vifungo vya miaka 30 kuanzia tarehe ya hukumu (wafungwa hao wawe wamekaa gerezani kwa miaka mitano na kuendelea kuanzia tarehe ya hukumu)
c. Wafungwa waliohukumiwa kunyongwa na kumaliza taratibu za kimahakama wabadilishiwe adhabu ya kifo na kuwa kifungo cha maisha.
d. wafungwa wazee wenye umri wa miaka 70 au zaidi ambao wamehukumiwa kifungo cha muda maalum /ukomo na waliokaa gerezani kwa muda wa miaka miwili na kuendelea.
e. Wafungwa wa kike walioingia na mimba gerezani au wenye watoto wanaonyonya
f. Wafungwa wenye ulemavu wa mwili na afya ya akili wasio na uwezo wa kufanya kazi
g.Wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kuwekwa kizuizini ambao wamekaa gerezani kuanzia miaka 10 au zaidi
h. Wafungwa wakike wasionyonyesha na walioko gerezani
i. Wafungwa wenye ulemavu wa akili
Aidha Msamaha huo HAUHUSISHI WAFUNGWA WAFUATAO
a.Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo gerezani kwa makosa ya uhujumu uchumi,matumizi mabaya ya madaraka,utakatishaji wa fedha, rushwa na usafirishaji au kujihusisha kwa namna yoyote ile na madawa ya kulevya ikiwemo bangi
b. wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo gerezani kwa makosa ya utekaji au wizi wa watoto,kupoka, kuwapa mimba wanafunzi na makosa yote yanayohusiana na ukatili kwa watoto na kujihusisha kwa namna yoyote ile na biashara haramu ya binadamu.
c. wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo gerezani kwa makosa ya kukutwa na viungo vya binadamu, unyang'anyi wa kutumia nguvu/ silaha,kumiliki silaha,risasi,milipuko au kujaribu kutenda makosa hayo.
d.Wanaotumikia vifungo gerezani kwa makosa ya kujihusisha kwa namna yoyote ile na nyara za serikali au ujangili
e. Wanaotumikia vifungo gerezani kwa makosa ya wizi au ubadhilifu wa fedha za serikali
f. Wanaotumikia vifungo kwa makosa ya kutoroka au kujaribu kutoroka chini ya ulinzi halali au kusaidia kutendeka kwa makosa hayo.
g. Wenye makosa ya kuua watoto wachanga, ugaidi,uharamia na makosa ya kimtandao
h. wanaotumika kifungo cha pili na warudiaji
i. Waliotenda makosa ya kinidhamu gerezani ambao makosa yao hayajatimiza mwaka mmoja mpaka kufikia april 26,2025
J. Wafungwa wa madeni
MUHIMU:- Kwa mamlaka aliyopewa chini ya Ibara ya 45 (1) (a) -(d) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inamruhusu Mhe. Rais kutoa msamaha huo na hatua hii ni katika kuadhimisha miaka 61 ya Muungano wa Tanzania tarehe 26 April 2025.