JOTOARDHI KUUNGANISHWA KWENYE GRIDI YA TAIFA
TANZANIA
Tanzania imelenga kuunganisha nishati ya jotoardhi kwenye Gridi ya Taifa ifikapo mwaka 2030 ili kuwa na umeme wa uhakika unaotokana na nishati jadidifu. (Hii ni kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Felchesmi Mramba katika mjadala wa viongozi kwenye mkutano wa Kimataifa wa nishati endelevu kwa wote (SEforALL) uliofanyika Jiji la Bridgetown nchini Barbados.).
Mpango huo ni miongoni mwa azma pana ya kuhakikisha upatikanaji wa umeme kwa wote ifikapo 2030 ili kuondokana na uzalishaji wa hewa ukaa ifikapo 2050.
Hii ni kutokana na sera ya Taifa ya Nishati ya Tanzania 2015 yenye Mpango Mkuu wa Nishati 2020 pamoja na Tamko la Dar es Salaam la 'Mission 300' katika mkutano wa nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika wa 2025.
Kupitia mpango huo mikoa 16 nchini itanufaika na maendeleo ya nishati ya jotoardhi, na kuifanya kuwa msingi wa mkakati wa nishati endelevu.