MUUNGANO UNAZINGATIA MISINGI YA UTAWALA BORA
DODOMA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Muungano wetu unaendelea kuzingatia misingi yautawala bora katika nyanja mbalimbali ikiwemo utawala wa kisheria,haki za binadamu uwazi, uwajibikaji na maridhiano.
Rais Samia ametoa kauli hiyo April 25, 2025 Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma wakati akilihutubia Taifa kupitia vyombo vya habari ikiwa imebaki siku moja kuelekea miaka 61 ya Muungano tarehe 26 April 2025.
Dkt Samia amesema"Muungano wetu unaendelea kuzingatia misingi yautawala bora katika nyanja mbalimbali ikiwemo utawala wa kisheria,haki za binadamu uwazi, uwajibikaji na maridhiano"
MIAKA61YAMUUNGANO