TSH BIL 54 KUJENGA NJIA 4 MBAGALA RANGITATU-KONGOWE

 

TSH BIL 54 KUJENGA NJIA 4 MBAGALA RANGITATU-KONGOWE

TSH BIL 54 KUJENGA NJIA 4 MBAGALA RANGITATU-KONGOWE

DAR ES SALAAM

Kiasi cha shilingi bilioni 54 kitatumika kwa ajili ya ujenzi wa barabara njia nne kwa kiwango cha lami kutoka Mbagala Rangi Tatu hadi Kongowe yenye urefu wa kilometa 3.8,  mradi ambao utatekelezwa kwa muda wa miezi 15 kuanzia Machi 19,2025  (uliposainiwa  mkataba)
Mradi huo unatekelezwa na mkandarasi kutoka nchini China, STECOL Corporation, na barabara hiyo ni sehemu muhimu ya miundombinu ya jiji la Dar es Salaam, ambapo kwa muda mrefu wananchi wamekuwa wakikumbana na foleni kubwa kuanzia Mbagala hadi Kongowe.
Kukamilika kwa ujenzi huo kutapunguza msongamano wa magari na kurahisisha usafiri kwa wakazi wa maeneo hayo na kuinua kiwango cha uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla, kuwezesha maendeleo na kurahisisha maisha ya wananchi.
KUMBUKA:- Hatua ya ujenzi wa barabara hiyo ni utekelezaji wa agizo  alilolitoa Mhe. Rais DKT Samia Oktoba 2023 aliposimama eneo la Mbagala na kuwasalimia wananchi akiwa anatokea kwenye ziara katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Pwani lengo likiwa ni kutatua changamoto ya foleni katika eneo hilo.
Aidha Agizo hilo lililenga kuhakikisha kuwa serikali inatekeleza miradi ya miundombinu kwa haraka ili kuboresha hali ya usafiri na kuongeza ufanisi wa shughuli za kiuchumi kwa wananchi.