UJENZI BARABARA YA TANGA-PANGANI YAFIKIA 75%

 

UJENZI BARABARA YA TANGA-PANGANI YAFIKIA 75%

UJENZI BARABARA YA TANGA-PANGANI YAFIKIA 75%

TANGA
Ujenzi wa barabara ya Tanga-Pangani umefikia asilimia 75 na inatarajiwa kukamilika Juni mwaka huu huku ujenzi huo ukigawanywa katika sehemu nne ili kuharakisha ujenzi wake.
Sehemu hizo ni Tanga-Pangani km 50, daraja la Pangani meta 525 na barabara unganishi km 25.6, barabara ya Mkange-Mkwaja-Tungamaa km 95.2 na sehemu ya Mkange-Bagamoyo Makurunge km 73.25 ambayo usanifu wake umekamilika.
Kukamilika kwa barabara hii kutachochea ukuaji wa uchumi, kupunguza gharama na muda wa safari, kuwezesha kufikika kwa urahisi vivutio vya utalii na kuunganisha kwa njia fupi bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mombasa