TANZANIA KUVUNA TSH BIL 663 ZA MAHINDI

 

TANZANIA KUVUNA TSH BIL 663 ZA MAHINDI

TANZANIA KUVUNA TSH BIL 663 ZA MAHINDI

DODOMA
Serikali ya Tanzania itavuna kiasi  cha shilingi bilioni 663 kwa kuuza mahindi nchini Zambia tani 650,000 za mahindi nchini Zambia kutokana na ukame unaoikumba nchi hiyo hatua iliyopelekea Tanzania kusaini makubaliano ya kuuza mahindi ili kuwasaidia wananchi milioni saba wa taifa hilo.
Mkataba huo utatekelezwa kwa kipindi cha miezi minane na mahindi hayo yatakayosafirishwa kwenda Zambia yatatolewa katika maghala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA). “Kituo cha Songwe kitatoa tani 55,000, Makambako tani 75,000, Sumbawanga tani 250,000 na Songea tani 270,000
Aidha pamoja na Zambia kununua tani 650,000 za mahindi kutoka Tanzania, Tanzania imeingia mkataba wa kuuza Tani 500,000 za mahindi kwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo(DRC) na mkataba wa kuuza tani 100,000 za unga wa mahindi WFP (Mpango wa Chakula Duniani) nchini Malawi.
Vilevile Mei mwaka huu NFRA ilisaini mkataba wa kuuza tani 500,000 za mahindi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). NFRA na kampuni ya Quincy ya DRC walisaini mkataba huo kwa ajili ya wananchi wa Jimbo la Katanga wanaokabiliwa na njaa.