VITONGOJI 9000 KUSAMBAZIWA UMEME 2025/2026
TANZANIA
Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inajipanga kufikisha umeme kwenye Vitongoji 9,000 katika mwaka ujao wa fedha wa 2025/26.
Hatua hii inakuja baada ya kukamilisha kazi ya kupeleka umeme kwenye Vijiji vyote Tanzania Bara na nguvu sasa inaelekezwa kwenye vitongoji.