TANGANYIKA YAPOKEA TSH BIL 4+ MIRADI YA MAENDELEO

 

pesa za miradi kwaajili ya watanganyika

TANGANYIKA YAPOKEA TSH BIL 4+ MIRADI YA MAENDELEO

KATAVI
Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan imeidhinisha jumla ya shilingi 4,175,800,000 kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Katavi.
Mgawanyo wa fedha hizo ni kama ifuatavyo sh bil. 3.51 zitajenga madarasa mpya 135, mil. 359 zitajenga vyumba vya madarasa ya mfano ya elimu ya awali 10, mil. 206.8 zitajenga matundu ya vyoo 94 na mil. 100 zitakarabati shule za msingi kongwe 2 katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika.