VITONGOJI 557 VYA RUVUMA KUPATA UMEME

 

VITONGOJI 557 VYA RUVUMA KUPATA UMEME

VITONGOJI 557 VYA RUVUMA KUPATA UMEME

RUVUMA
Serikali imejidhatiti kuhakikisha wananchi wanapata umeme hususani katika vitongoji 557 vya Mkoa wa Ruvuma.
Tanzania ina vitongoji takribani 64,000, na hadi sasa wamefanikiwa kupeleka umeme kwenye vitongoji 33,000.
Wakati serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inaingia madarakani, kulikuwa na vijiji 4,071 visivyokuwa na umeme na hadi sasa vijiji vyote nchini vina huduma ya umeme huku  serikali ikielekeza nguvu kuhakikisha umeme unafika kwenye vitongoji ambapo vitongoji 557 katika mkoa wa Ruvuma vitanufaika na mradi huo wa kufikishiwa umeme katika awamu ya kwanza ambayo inatarajiwa kuanza hivi karibuni.
Aidha,  Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amejitanabaisha katika matumizi ya nishati safi ya kupikia ambapo serikali chini yake imeagiza  ifikapo mwaka 2030, asilimia 75 ya wananchi wawe wanatumia nishati safi ya kupikia, na asilimia 80 ifikapo mwaka 2034.
MUHIMU:- Tafiti zilizofanywa zimeonesha kuwa matumizi ya nishati safi ni rahisi zaidi kuliko matumizi ya nishati isiyo safi kama mkaa na kuni, ambazo gharama zake ni kubwa ukilinganisha na nishati safi ambapo Serikali inaendelea kuhamasisha wananchi kutumia nishati safi kwa manufaa ya afya na mazingira.