TSH BIL 27 KUBORESHA AFYA NCHINI

 

TSH BIL 27 KUBORESHA AFYA NCHINI

TSH BIL 27 KUBORESHA AFYA NCHINI

DAR ES SALAAM
Tanzania na Japan kupitia Shirika la Maendeleo (JICA), zimetiliana saini mkataba wa msaada wa shilingi bilioni 27.3 kwa ajili ya kuboresha sekta ya afya nchini.
Mkataba huo umesainiwa jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dk Natu El-maamry Mwamba, kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Yoichi Mikami na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), Hitoshi Ara, kwa niaba ya Serikali ya Japan.
Fedha hizo zitatumika katika ununuzi wa vifaa-tiba ili kuimarisha huduma za afya ya mama na mtoto katika hospitali saba ambazo ni Dodoma, Tumbi iliyoko mkoa wa Pwani, Mount Meru iliyoko Arusha, Sekou-Toure iliyoko Mwanza, Songea iliyoko Ruvuma, Maweni iliyoko mkoani Kigoma na Hospitali ya Lumumba iliyoko Zanzibar.
Aidha ufadhili huo muhimu unaendana na Mpango wa sasa wa Maendeleo wa Miaka Mitano ambao pamoja na masuala mengine, unalenga kutatua changamoto za ubora katika utoaji huduma za afya nchini