BANDARI YA MBAMBABAY KUKAMILIKA 2026
RUVUMA
Ujenzi wa bandari mpya ya kisasa ya Mbamba Bay inayojengwa pembezoni mwa Ziwa Nyasa katika wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma inayotumia gharama kiasi cha shilingi bilioni 7.8 inatarajiwa kukamilika Januari 2026 ambapo hadi sasa ujenzi wake umefikia asilimia 6 na unatakelezwa na mkandarasi Xiamen Ongoing Construction Group Limited na mshauri (Consultant) Anova Consult.
Utekelezaji wa ujenzi wa bandari hiyo utahusisha ujenzi wa gati mbili zenye urefu wa mita 103 ,ujenzi wa maghala, nyumba za watumishi, jengo la utawala, jengo la abiria, karakana, mnara wa tanki la maji na jengo la huduma za afya.
Pia kutakuwa na ujenzi wa daraja lenye urefu wa mita 105 na upana wa mita 15 kwa ajili ya magari ya kubebea mizigo na eneo la kuhifadhia makontena 3,000 ya mizigo.
Ujenzi pia utahusisha barabara za ndani na nje ya bandari kwa ajili ya magari kuingia na kutoka bandarini hapo.
Ujenzi wa bandari hiyo utasaidia usafirishaji wa haraka wa mizigo, zikiwemo bidhaa za viwandani, mazao ya kilimo na uvuvi mizigo kwenda nchi jirani za Msumbiji, Malawi, na Zambia zikitokea bandari ya Mtwara kupitia Ziwa Nyasa
Hadi sasa serikali kupitia TPA imeshamlipa mkandarasi mjenzi malipo ya awali (Advance Payment) kiasi cha shilingi 3,261,529,017.63 sawa na asilimia 5 na kumlipa Mhandisi Mshauri kiasi cha shilingi 448,192,240.70 kama malipo ya awali ambayo ni sawa na asilimia 10.
ZINGATIA HAPA:- Dhamira ya Serikali ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ni kujenga miundombinu ya kisasa katika bandari zote hapa nchini, ili kukuza uchumi na kutoa ajira kwa Watanzania.
