HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA KASKAZINI (KCMC)

 


HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA KASKAZINI (KCMC)  

Serikali ya awamu ya sita katika kipindi cha miaka minne imewekeza Shilingi Bilioni 5 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kituo cha tiba mionzi pamoja na ununuzi wa vifaa tiba katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Kaskazini (KCMC) iliyopo Moshi Mkoani Kilimanjaro ili kuboresha huduma hizo za afya na kuwafikia wananchi wengi wa ukanda huo.
Kituo hicho cha tiba mionzi kitakuwa ni kati ya vituo vichache ambavyo vinatoa huduma za matibabu ya ugonjwa wa saratani kwa njia ya mionzi kutoka kwa wataalam wenye ubobezi na umahiri wa hali ya juu wa hapa nchini kwetu ambao wamesomeshwa kupitia ufadhili wa Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
#BimkubwanaAfyakazini