HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA

 


HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA

Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH)  iliyopo Mkoani Dodoma kwa kipindi cha miaka minne  imetoa huduma za matibabu kwa watu 970,000  huku ikiendelea kuimarisha huduma za kibingwa na ubingwa bobezi ili kuboresha afya za Watanzania.
Hospitali hiyo kwa kipindi cha miaka minne  imefanikisha upandikizaji wa figo kwa wagonjwa 250, huku wagonjwa wengine 10 wakinufaika na huduma hii kupitia mfuko maalumu wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Aidha, Serikali imetumia kiasi cha Shilingi Bilioni 1.4 kutoka katika Mfuko Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya upandikizaji wa uloto kwa watoto wenye ugonjwa wa selimundu. 
Katika kuboresha huduma za uchunguzi na matibabu ya mfumo wa chakula, hospitali ya Benjamin Mkapa imeongeza vifaa tiba vya kisasa na kusomesha wataalam, hali inayochochea kuhudumia zaidi ya wagonjwa 10,000 katika eneo hilo.
Halikadhalika Hospitali ya Benjamin Mkapa imeongeza upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kutoka asilimia  68 mwaka 2022 na kufikia asilimia 96 mwaka 2025 hii ni kutokana na kuongeza kwa bajeti ya dawa   pamoja na Serikali na kufungua vituo vya dawa katika hospitali.

#BimkubwanaAfyakazini