TSH BIL 2.2 ZAJENGA SHULE 4 ZA SEKONDARI MBINGA
RUVUMA
Serikali kuu imetoa kiasi cha shilingi 2,242,211,308 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma kwa ajili ya ujenzi wa shule nne mpya za sekondari katika mwaka wa fedha 2024/2025.
Shule hizo zimejengwa katika kata za Nyoni, Litembo, na Muungano, ambapo tayari zimekamilika na zimeanza kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza tangu Januari 2025 na Shule moja inajengwa katika Kata ya Langiro, na ujenzi wake unaendelea.
Katika hatua nyingine ya kuboresha elimu, Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ilipokea walimu 36 wa masomo mbalimbali mwezi Februari 2025, na tayari wameripoti katika vituo vyao vya kazi.