UJENZI HOSPITALI YA RUFAA KUSINI KUANZA APRILI 2025
MTWARA
Serikali imetenga Sh bilioni 3 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa awamu ya pili wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini mkoani Mtwara, ambapo ujenzi huo unatarajiwa kuanza Aprili 2025.
Hadi hivi sasa taratibu za kumpata mkandarasi zimeanza hata hivyo zabuni imeshatangazwa na baada ya wiki mbili watakamilisha hatua hiyo.
Usanifu wa michoro umeshakamilika na tayari taratibu za kumpata mkandarasi zimeanza, huku zabuni ikiwa imeshatangazwa, na ndani ya wiki mbili itakuwa imekamilishwa.
Kiasi hicho cha fedha kitatumika kujenga jengo la mama na mtoto, nyumba za watumishi, kichomea taka, na jengo la kufulia.
Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini inatoa huduma za kibingwa kwa wananchi wa mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma, na maeneo jirani.